Saturday, May 06, 2006

KWA NINI HOTBUBA NA UTEKELEZAJI WA IRANI YA UCHAGUZI UNAOFANYWA NA MH. JK HUIBUA HARI YA TABAKA KATI YA MATAJIRI VIONGOZI NA MASIKINI WANYONYWAJI

Tafakari za Maisha
Ninayofuraha kubwa kupita kisiwani hapa na kutoa salaam zangu kwa wana kisiwa baada ya kupotea kwa muda.Sikuwa na cha kushangaza sana ila tu ni shughuli za kimasomo.Hivyo nimeona nipite hapa japo kwa vijisiku vichache nilivyo navyo.
Tukirudi kwenye mada husika ni majuzi tu mkoani hapa tulipata bahati ya kutembelewa na mh. Rais ikiwa ni moja ya sehemu ya ziara yake ya kuzunguka nchi nzima kusema asante kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa jamuhuli ya muungano wa Tanzania.Sina kipingamizi juu ya hili na ni utamaduni mzuri kusema asante.
Kama ilivyo kwa wengi imekuwa ni kama desturi sasa ya Mh JK kusikika akitoa onyo ama kuadabisha baadhi ya watu au watumishi wa idara mbali mbali juu ya utendaji wao mbovu au maovu wayafanyayo katika jamii inayo wazunguka.Mwenyezi Mungu amjalie Mh huyu utamaduni huu uwe sehemu ya maisha yake ya kila siku
Katika hotuba yake mkoani hapa Mh JK aliahidi kuboresha uduma za afya,kuongeza barabara za rami na kusambaza maji.kwa upande wa utendaji mkoani hapa ilikuwa kinyume kabisa kwani Rais alitamka wazi wazi kwamba halmashauri yetu imejaa mchwa ambao uwezo wao wa kutafuna sio kwenye mbao tu bali wanao uwezo hata wa kutafuna paa za majengo ya ofisi.Hotuba ilisitishwa kwa makofi na vifijo pale Rais alipo toa tamko lake kama mwanzo wa utekelezaji wake kwa kuanzia na wizara ya aridhi ametoa siku 30 kuakikisha viwanja vyote vilivyo gawiwa kwa mtu zaidi ya mjoja kuorodheshwa na wahusika walio saini kugawa viwanja hiyo wachukuliwe hatua bila kujali wako mkoa gani kwa sasa.Huu ni mwanzo mzuri tusubili mwisho wake kwani ili halitaishia hapo tu ikizingatiwa kwamba halimashauri yetu iko katika nafasi nzuri tu miongoni mwa zile halmashauri zinazo tuhumiwa kwa kula pesa za "mem" yaani mpango wa kuboresha elimu ya msingi zitolewazo na whisani..
Wasi wasi wangu ni kwamba ukweli huu unapo ongelewa bayana wengi kati ya wale wanaofurahishwa na ukweli huu ni lile tabaka la chini kabisa na kwa walengwa yaani watuhumiwa uonekana kama chuki binafsi,na ni hapo hapo utakapo anza kusikia chini kwa chini mbona hata yeye mwenyewe ni yale yale.sikatai yawezekana ukawa sahihi lakini kumbuka si kweli kwamba kosa likifanywa na wengi si kosa na kwamba sheria inaweza kupindishwa kama kosa limefanywa na wengi,La hasha.Tubadilike tumuunge mkono Rais wetu juu ya mchakato mzima wa kuitekeleza ilani ya uchaguzi ambayo ni maisha bora kwa kila mtanzania.Na hili ni kwa wote viongozi na wasio viongozi.Nafikiri ni bora kuwa na kiongozi aliyetayalikusikia na kukubali kukumbushwa kwa yale aliyo ahidi kuliko kuwa na kiongozi ambaye anatanguliza jaziba na ukari ilikufiha uozo wake..