Sunday, January 15, 2006

KANISA KATORIKI KUPINGANA NA SERIKALI

Kanisa Katoriki limepinga kufundiswa kwa mtaala mpya juu ya mambo ya kujamiiana na matumizi sahihi ya namna ya kutumia kondomu kwa wanafunzi wa darasa la nne kwa madai kwamba wanafunzi hao ambao wengi wao ni kati ya miaka kumi na mbili hadi kumi na nne kuwa hawastahili kupewa elimu hiyo.
Swali je hao ambao wanadhaniwa kustairi mafunzo hayo yanawasaidia?Je bado kuna haja kwa jamii zetu kuendelea kufanya siri ya kutoongelea waziwazi kuhusu mambo ya kujamiana na athari zake?Tuchukulie kwa mfano katika familia unaweza kukuta baba ananyumba ndogo lakini kwa kuwa ni jambo la siri sio rahisi kwake kukubali kuulizwa na mkewe na hapa kinachofuata kama mama atakuwa amebaini hilo mama nae atatafuta namna ya kutoka nje kwa siri na kinachofuata kutokana na usiri huo ni UKIMWI.Na watoto kwa kuwa tayari wanalo jina la ubatizo kinachofuatia ni wao kuitwa watoto yatima.
Lakini kama tungelikuwa na kukuta swala hili linaongelewa wazi wazi ni dhahiri hata watoto wangeliwaomba wazazi wao kuchukuwa tahadhari juu ya ugonjwa huu hatari iliwasije kufa na kuwaacha yatima bila mbele wala nyuma, na ombi hili kwa wazazi lingelionekana kama maombi mengine ambayo mtoto anaomba kutoka kwa wazazi wake.sasa kwa kuwa sisi hatukupata fulsa hii basi tuwaache hawa tunaosema ni wadogo wapewe elimu hiyo pengine inawezekana ikawa ndio mwanzo wa swala hili kuongelewa katika ngazi ya familia kwa sababu watoto wataitaji kuwaeleza wazazi wao kile walichojifunza shuleni na hapa sasa ndio wakati muafaka kwa mzazi kutoa mafunzo sahihi na hata ushauri unaofaa kwa mwanae.kwa sababu wazazi wengi hawana ujasiri wa kuliongelea swala hili kwa watoto wao zaidi wakijitahidi watesema tu kwa ufupi bwana sikuizi kuna ukimwi angalia!!sasa hapa ajawa wazi ni angalie nini?au ni fanye vipi ilikukabiliana na tatizo?Karibuni tujadili.

10 Comments:

At 6:58 PM, Blogger Ndesanjo Macha said...

Ndugu yetu, hivi una kiungo chochote cha habari kamili kuhusu kanisa katoliki na serikali?
Safi sana umevunja ukimya kwa nguvu.

 
At 1:03 AM, Blogger mark msaki said...

kwa kweli hapo ni pagumu. wakati kanisa linapigania kujenga morali ya wananchi la takiriba zinaaa serekali inapambana watu watumie zana. mie nadhani kitendo cha kanisa kuingilia kupanga umri wa watoto kuanza kufundishwa kuhusu kondomu ni hatua ya kwanza kukubali matumizi yake. mimi nadhani lingekaa kimya au kupinga moja kwa moja ili ijulikane msimamo wake. misingi isiyobadilika ya kanisa katoliki ni muhimu sana katika dunia inayobadilika kasi...rejea ndoa za mashoga.

 
At 2:16 PM, Blogger John Mwaipopo said...

Siku zote kanisa katoliki ni nafiki. Rafiki yangu mmoja, naye mkatokiki kama mimi, analiita 'akili kichwani'. Wamekuwa wakitawala serikali za dunia kisirisiri pasi na sisi kujua.

Ndio maana utawasikia mara ooh kiongozi fulani anafaa kuwa mtakatifu. Ukiona hivyo ujue huyo aliongoza kwa misingi ya kanisa na kuwapigia magoti.

Ndesanjo: Asante kwaa Kitabu kilichopigwa marufuku Tanzania.Nimekisoma choote. Ingawaje kina uongo fulani lakini sehemu zingine ni ukweli ulio uchi kabisaaaa. Kimeniongezea ufahamu.

 
At 3:22 AM, Blogger Indya Nkya said...

Ungetupa kiungo kingesaidia sana. Kwa sababu pengine swali langu lingejibiwa; kwamba wamependekeza kifanyike nini? Nadhani kanisa linachukulia kwamba watoto wa umri huu hawafahamu chochote kuhusiana na mambo ya ngono. Tafiti zinaonyesha kwamba watoto wengi huanza ngono wakiwa na umri wa miaka kuanzia 12!!

 
At 4:02 AM, Anonymous ndesanjo said...

Umeishilia cha wapi?

 
At 9:06 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Masuala haya ya ukimwi yananiumiza kichwa sana kila kukicha.Mwaka huu ule mkutano wa umoja wa mataifa kuhusu ukimwi unafanyikia hapa Toronto kufuatia ule wa Barcelona.Nitahudhuria na pengine dunia itaniona kwani napanga kuongelea suala nyeti la tamaduni zetu za kiafrika,dunia yetu ya sasa,ukimwi kama tatizo la utandawazi.Kama kuna mahali ambapo tumekwenda mrama basi ni pale tulipokubali uongo kwamba tamaduni zetu ni mbaya kisha tukaanza kuzivalisha blanketi hizi za kimagharibi.Makanisa na imani zinasahau kwamba kinga kubwa kuliko zote ilikuwa tamaduni zetu,Zile ambazo mwali alikuwa mwali,kigori alikuwa kigori na mseja alikuwa mseja.Nini kimetokea?Mimi nasema uzungu umetukabili.Mzazi alimwachia shangazi au bibi amfunze mwana kuhusu kujamiiana,ilikomea wapi hiyo?Shule za leo zitafundisha nini?Zitaonya kuhusu nini?Mimi najua zitakachosema,nendeni mkafanye,ni haki yenu,lakini kuweni makini,tumieni hizi zana.Je huu ni utamaduni wetu.Utamaduni wetu ulikuwa na kasoro gani?Mbona hatukai chini na kuhoji masuala haya kwanza?

 
At 1:59 PM, Blogger Boniphace Makene said...

Mujarifu umepotelea wapi, tumekumis sana hadi tunachoka kusoma kutoka Musoma.

 
At 5:24 AM, Blogger Mikundu Matako Makalio Manundu said...

Duuuhhhhh, hebu jipumzisheni na siasa kwa kumtembelea Mzee Mikundu kwenye blogu yake,

http://mikundu.blogspot.com/

Kidogo mjiliwaze na hayo ma-text marefu marefu. Tazameni Mikundu, Matako mpate kupiga punyeto vizuri, kwani wanasema mkono una-raha kuliko kuma, mkundu, mdomo, kwapa, Jee kweli?

 
At 4:07 AM, Anonymous Vimax Asli said...

thanks for nice sharing and good information

 
At 7:12 AM, Anonymous Vimax Canada said...

That's what everyone likes. You have a good imagination. Great post thanks you

 

Post a Comment

<< Home