Sunday, January 15, 2006

KANISA KATORIKI KUPINGANA NA SERIKALI

Kanisa Katoriki limepinga kufundiswa kwa mtaala mpya juu ya mambo ya kujamiiana na matumizi sahihi ya namna ya kutumia kondomu kwa wanafunzi wa darasa la nne kwa madai kwamba wanafunzi hao ambao wengi wao ni kati ya miaka kumi na mbili hadi kumi na nne kuwa hawastahili kupewa elimu hiyo.
Swali je hao ambao wanadhaniwa kustairi mafunzo hayo yanawasaidia?Je bado kuna haja kwa jamii zetu kuendelea kufanya siri ya kutoongelea waziwazi kuhusu mambo ya kujamiana na athari zake?Tuchukulie kwa mfano katika familia unaweza kukuta baba ananyumba ndogo lakini kwa kuwa ni jambo la siri sio rahisi kwake kukubali kuulizwa na mkewe na hapa kinachofuata kama mama atakuwa amebaini hilo mama nae atatafuta namna ya kutoka nje kwa siri na kinachofuata kutokana na usiri huo ni UKIMWI.Na watoto kwa kuwa tayari wanalo jina la ubatizo kinachofuatia ni wao kuitwa watoto yatima.
Lakini kama tungelikuwa na kukuta swala hili linaongelewa wazi wazi ni dhahiri hata watoto wangeliwaomba wazazi wao kuchukuwa tahadhari juu ya ugonjwa huu hatari iliwasije kufa na kuwaacha yatima bila mbele wala nyuma, na ombi hili kwa wazazi lingelionekana kama maombi mengine ambayo mtoto anaomba kutoka kwa wazazi wake.sasa kwa kuwa sisi hatukupata fulsa hii basi tuwaache hawa tunaosema ni wadogo wapewe elimu hiyo pengine inawezekana ikawa ndio mwanzo wa swala hili kuongelewa katika ngazi ya familia kwa sababu watoto wataitaji kuwaeleza wazazi wao kile walichojifunza shuleni na hapa sasa ndio wakati muafaka kwa mzazi kutoa mafunzo sahihi na hata ushauri unaofaa kwa mwanae.kwa sababu wazazi wengi hawana ujasiri wa kuliongelea swala hili kwa watoto wao zaidi wakijitahidi watesema tu kwa ufupi bwana sikuizi kuna ukimwi angalia!!sasa hapa ajawa wazi ni angalie nini?au ni fanye vipi ilikukabiliana na tatizo?Karibuni tujadili.

Wednesday, January 11, 2006

INAWEZEKANA KABISA KAMA TU TUTASEMA TUNACHO MAANISHA NA KUTENDA KWA VITENDO KILE TUNACHOJIPANGIA KUTOKA KATIKA HISIA ZETU

Kama isivyo wezekana kwa binadamu kuota ndoto pasipo na usingizi,vivyo hivyo ni ngumu kabisa kwa karne hii kwa mtu yeyote yule anyekusudia kwa kila hari kutimiza adhma yake kwa kile alicho jipangia na kujitumainisha kwacho kama daraja na kivuko imara dhidi ya mkondo kasi wa maji ya umasikini ulio kithiri.Na kama ilivyo katika viungo vya mwili hakuna hata kimoja kinacho thubutu kutegea kiungo kingine na kana kwamba hiyo haitoshi viungo hivi vya mwili ushiliki maumivu na shida ipatikanayo katika kiungo kimojawapo.Kwa hiyo kama hivyo ndiyo basi malengo na ndoto zetu juu ya kesho iliyo bora na yenye nafuu zaidi ya jana hazina budi kwenda sambamba na tahadhari endelevu dhidi ya ugonjwa hatari wa UKIMWI.Ni ngumu sana kuchukua tahadhari yakinifu na endelevu juu ya swala hili ndani ya mtu hasa pale unapo hisi na kujiona mwenye afya njema na furaha wakati wote na pia huwa ngumu zaidi pale ambapo utabaini kuwa siyo tatizo kwako kumudu gharama za maisha yako ya kila siku sambamba na kutoikosa mitoko ya mwisho wa wiki,sikatai ni kweli furaha ni sehemu ya maisha na kufurahia maisha sio dhambi,ila mtakubaliana na mimi kuwa robo tatu ya yale yanayo tendeka katika sehemu mbambali za starehe ni virutubisho sahihi vya tatizo hili(UKIMWI)Je unasherekea na kufurahia salama?au unarutubisha tatizo hili?Na pia ni rahisi mno kuhisi ushindi wa bwerere dhidi ya vita hii hatari kwa kuamini kutoka moyoni kuwa wewe si kama wale unoupendeleo fulani ambao unafikili utakushitua kabla ya wewe kujiunga na kundi lile ambalo linaishi kwa matumaini na siyo matumaini tu bali linaouhakika wa kumaliza ungwe yao mapema kabla ya muda wa kawaida wa mchezo kumalizika.Na kama invyofikirika na wengi katika fikra zetu kuwa ni ngumu kujitoa na kujitenga na yale yanayo aminiwa kuwa ni chachu na chanzo cha gharika hili.Lakini mambo ni tofauti kabisa kwa upande wa pili wa sarafu ni rahisi kabisa kwa yule aliye kwisha nasika kutimiza hayo yote bila shida endapo tu atapewa nafasi ya pili na Mwenyezi Mungu katika maisha yake hapa Ugenini(duniani).Ni mjadala ambao pengine unaweza kuwa hauna mvuto kwa haraka haraka na hili ni kwa sababu sawa hili linahitaji utayali wa mtu binafsi katika kulifanikisha,lakini kama kweli tumeamua kama wan blogu kuakikisha ifikapo elfu mbili na kumi kuwa mwaka wa mabadiliko basi hatuna budi kwenda sambamba na hii vita dhidi ya adui mkubwa UKIMWI.Kama ilivyo kwa familia yeyote ile inapokumbwa na tatizo hilihujikuta ikikabiliwa na bajeti isiyo rasmi lakini ya lazima na isyo kwepeka na gharama hizi ni kwa ajili ya matibabu ya mtu mmoja na matibabu haya uhitimishwa na gharama kubwa kabisa za mwisho ambazo si uzima bali ni mauti ya mgonjwa na shughuli nzima ya kumstili mwili wake.sasa kama familia uzaa kaya na kaya uzaa kata na kata uzaa wilaya na wilaya uzaa mikoa na mikoa uzaa taifa na taifa ndio mimi na wewe je nikipi basi kitakacho tunusulu kutoka kwenye gharama hizi kubwa ambazo kila kukicha waanga wake wanongezeka mamia kwa mamia?na sasa cha kusikitisha na kuuzunisha ni hili kundi ambalo hapo awali lilitumainiwa kuwa mkombozi lakini sasa wana ndoa nao imekuwa ngumu kwao kutoshelezana ndani ya ndoa zao na sasa wanaomba siti kwa kasi kabisa mbele ya msafara wa kundi la vijana ambao wameonekana kushindwa na kutotaka kuchukua tahadhari makini juu ya swala hili.Je ni kweli wanandoa wanacho kitafuta nje ya ndoa zao ni bidhaa hadimu katika nyumaba zao?Je ni kweli kwamba vijana tumeshindwa kabisa kufuata matumizi sahihi ya kinga zilizopo dhidi ya tatizo hili au ndio kusema thamani ya utu wetu hatuijui na kama hatuijui iweje basi tunatamani kuishi na kufikia malengo yetu inhali hatuko tayalri kupambana na tatizo hili?Ninaomba niishie hapa lakini wito wangu kwa wana blgu wote kama ilivyo kwa mada nyinginezo zenyekuifumbua macho jamii basi nafikiri hili ni muhimu pia kupewa uzito unaostahili ili Afrika iwe ni sehemu ya kuishi watu na si makaburi.

Tuesday, January 03, 2006

JE NI KWELI SWALA HILI LAWEZA KUWA KIKWAZO KATIKA UTENDAJI WA PCB?

Nimekuwa nikjiuliza maswali bila kupata majibu ya moja kwa moja juu ya swala zima la ruswa hapa nchini,itakuwaje mazingira ya ruswa yanajibaini wazi wazi na kana kwamba hiyo haitoshi mashairi ya kuomba rushwa yamekuwa yakiongezeka siku hadi siku katika secta za serikali na binafsi pia utasikia toa chai, mara soda,mara ongea vizuri.
Itakumbukwa kwamba wakati wa mh.mkapa iliundwa tume ya kupambana na ruswa hapa nchini(PCB)lakini cha kushangaza tume hii imekuwa inakosa ushaidi wa kutosha kumtia mtu hatiani.Wengi tumeshuhudia katika kipindi kilicho pita katika chaguzi hapa nchini Tanzania,wengi kati ya wagombea wa nafasi mbali mbali walitumia pesa zao kutafuta madaraka na dhamana ya kuiongoza nhi hii na ikama mtakumbuka hata Mh.Rais wa sasa aliliongelea katika hotuba yake ya kwanza kwa bunge.Kuwa anajua yakwamba wapo viongozi miongoni mwa wale waliokuwa wakimsikiliza ambao walitumia pesa kupata madaraka.Sasa swali linakuja hii tume ya kudhibiti rushwa inashindwaje kuwatia hatiani watu au viongozi kama hawa?Je kunahaja ya hii sheria ya rushwa kufanyiwa malekebisho kwa sababu kwa mujibu wa sheria mtoaji na mpokeaji ruswa wote wawili wanahatia kisheria sasa itawezekanaje kumtia mtoa ruswa hatiani inhari mpokeaji hayuko tayari kutoa ushaidi wa kupokea ruswa kutokana na sheria ya nchi kumbana yeye pia.Nafikiri ni muda muafaka sasa kuitazama upya sheria hii ya ruswa vinginevyo PCB itaendelea kuwepo na ruswa itaendelea kushamiri.

HERI YA MWAKA MPYA KWA WANABLOGU WOTE

Nichukue fulsa hii kuwatanieki heri ya mwaka mpya wana blogu wote popote pale mlipo,Ndio ni kweli kabisa ni kimya kimepita baada ya kujitambulisha katika ulingo huu.Tatizo lilikuwa ni la kiuufundi sikuwa nikiweza kuweka makala mpya katika ukurasa wangu na haikuwa rahisi kwangu kugundua tatizo lilikuwa wapi.ila kwa sasa ninaona limekwisha na tutakuwa pamoja tena.