Tuesday, December 20, 2005

NILIPI LA MUHIMU KWANZA KATI YA HAYA MAWILI

Ni alfajiri ya takribani saa kumi na mbili kasoro,kama ilivyo ada ninakifungulia kiredio changu ili kupata udaku unaoendelea duniani.Lakini moyoni ninahisia ya baadhi ya mambo ambayo pengine nitayasikia pindi tu nitakapo kuwa nimekifungua kiredio changu, kama matokeo ya uchaguzi wa madiwani,wabunge na raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.bila kusahau uonevu alioukili mfalme Bush dhidi ya inch ya Iraq na washukiwa wa makosa ya ugaidi.Sina wadhifa wowote katani hapa na pia si mfuasi wa chama chochote cha kisiasa ila ni mfuasi wa mgombea atakayekuwa na uchungu na inchi hii pamoja na rasilimali zilizomo na pia awe tayari kuwa kiongozi na mtumishi kwa wana inchi na asiwe mtawala.Kama ilivyo kwa wanakata wenzangu ninaamini kabisa kwamba mmoja kati ya wagombea uraisi wa chama furani lazima atashinda kiti hiki cha uraisi kwani chama chake ndicho chenye dhamana kwa sasa ya kumiliki vyombo vyote muhimu hapa inchini,kama vile jeshi,polisi na hata mahakama zote, na sababu nyingine ni mtu aliye tokea kupendwa tu jambo ambalo wengi wa wafuasi wake ukiwauliza nini alicho ifanyia Tanzania cha pekee kinacho mnusuru na dhambi walizo nazo viongozi wenzake.Lakini nimekuwa nikijiuliza bila majibu jumla ya gharama alizo zitumia bwana huyu katika kapeni yake ya uraisi ni kubwa sana ukilinganisha na ya wagombea wenzake.Najiuliza je bwana huyu akiwa raisi atakuwa na uchungu na fedha ya wanainchi?je ataweza kuwajari akina mama wajawazito na watoto dhidi ya adui mkubwa marelia?ikiwa fedha aliyo tumia kutengeneza tisheti na kofia kwa inchi nzima ingeweza kuwanunulia akinamama wajawazito vyandarua kwa inchi nzima wakiwemo watoto wa chini ya umri wa miaka mitano,hapa ninaingiwa na wasiwasi juu ya ahadi zake nyingi alizo waahidi wanainchi.Gafra ninashutka ni saa moja na kibaruani ninatakiwa kufika saa moja na nusu hivyo nina shika njia huku nikiwa ninajaribu kujihoji ni kipi cha muhimu kwanza kati uhai na kuvaa.

9 Comments:

At 7:36 AM, Blogger Boniphace Makene said...

Nafurahi kuwa wa kwanza kabisa kuchagia katika mjadala wa blogu yako. Kweli nchi ni yetu lakini yatafunwa na wajanja wachache. Kinachgotakiwa kufanyika ni mimi na wewe kuwaunganisha wwenzetu tufungue blog hizi kwa sana ili jamii iweze kusoma na kujua yanayoendelea maana vyombo vya habari vya nyumbani vinanyima ukweli au vinafunika baadhi ya mambo na hapa unalala nao moja kwa moja hakuna wa kukuliza maana unalo soko lisilo na mipaka. Karibu mjarifu karibu sana, wewe mwanazuo pia na hili tafakari lako la maisha laonekana kuja kiriwaya na siku si nnyingi inshalah litatisha sana.

 
At 11:54 PM, Blogger Phabian said...

Asante sana bwana boniface kwa kunikaribisha katika uwanja huu mimi ninauita uwanja wa mapambano.Natumaini tutakua pamoja pega kwa pega kuifanikisha azma yetu ya kuwekana sawa juu ya mambo kadha wakadha.

 
At 10:55 PM, Blogger mark msaki said...

Phabian,

kweli wewe ni mwanafasihi. uliyoyasema yanawakilisha mawazi mengi tu ya watanzania! lakini ni watanzania hao hao pengine hawajui sababu ni nini. katika fasihi hii inaonekana kuwa huyu mwananchi ameanza kupata pata mwanga kwa kuoanisha maisha yake na chaguzi anazozifanya yeye mwenyewe kupitia sanduku la kura!!! huyu ana ahueni na mungu saidia kufika 2010 anaweza kuwa mwenye kufanya maamuzi sahihi zaidi juu ya maisha yake! la kusikitisha sasa ni pamoja na kuhisi kwake kuwa kunaweza kusiwe na uwiano kati kuvaa na kula, pengine hataweza kufanya maajabu sana kwani waangalizi ndo hao wamebariki matokeo, raisi kashaapishwa na wabunge ndio wanaingiza timu dom kwa spidi ya tsunami! cha msingi sasa, tusibweteke kwa maneno ya watwawala kuwa uchaguzi umekwisha tujenge nchi!! sawa sie tunajenga kwa kuamsha umma ili safari ijayo t shirt zisitumalize!! upinzani unahitaji makada!! karibu na karibisah wenzako tunoane halafu tupande majukwaani!

 
At 5:10 AM, Blogger mloyi said...

Nadhani na wewe pia unatafuna pesa za serikali! Unawezaje kutoka nyumbani saa moja ufike kazini saa moja na nusu? au wewe ni mhindi?. sisi huwa tunatoka nyumbani saa kumi na mbili tufike kazini saa moja na nusu.
Kula au kuvaa! chagua moja. Kama vile wengine wanavyochagua kuwa na kazi au kutokuwa na kazi, usicheke, unaweza kama na wewe pia ni juha kama wale jamaa wa jana.
Unajua huyu jamaa alifanya kampeni mpaka saa nane usiku, watu hawajui alikuwa analala saa ngapi,walijaribu kumzuia lakini aliwakatalia. tunaombea afanye kazi hivyohivyo bila kuzuiliwa na mtu asiyetutakia mema. Ndiyo tutajua lipi bora kati ya kula na kuvaa.

 
At 8:08 AM, Blogger Jeff Msangi said...

Karibu sana uwanjani.Kilio chako cha lipi la maana zaidi kati ya maisha au kuvaa linajibika kwa hoja kwamba aliyeshiba hamjali mwenye njaa.Tusitegemee jipya kutoka kwa wanasiasa hawa.Nguvu ya mwananchi ndio muhimu.

 
At 5:02 AM, Anonymous nyembo said...

TEHETEHE!!!nacheka,nafurahi....sicheki kicheko kisicho sababu! nasema nimesema kuwa nimefurahi nani anabisha!wewe Makene au Wasangi wote walio wa msangi...Phabian ni shujaa ni kweli.kwa maana kaanza kwa mapambano si lelemama huku si sehemu ya soga isiyo na hoja.aliyelala lazimaataamka na kuamsha wengine hapa nasema muhimu si kufungua Blog yako kaka ni Muendelezo wa hoja zilizo moto na ufunguzi wa kifikra kwa msingi wa kuandika karibu kaka!!!!!!!!!

 
At 8:30 AM, Anonymous Pelangsing cepat alami said...

thanks for sharing nice blog and good information

 
At 4:56 AM, Anonymous alat bantu sex said...

thank you sir for the news you give this. really very good indeed. and I want to add a little bit of information specifically for adult men and women.

 
At 7:06 AM, Anonymous Vimax Canada said...

That's what everyone likes. You have a good imagination. Great post thanks you

 

Post a Comment

<< Home