Wednesday, December 21, 2005

Tafakari za Maisha: NILIPI LA MUHIMU KWANZA KATI YA HAYA MAWILI

Tafakari za Maisha: NILIPI LA MUHIMU KWANZA KATI YA HAYA MAWILI

Tuesday, December 20, 2005

Tafakari za Maisha: NILIPI LA MUHIMU KWANZA KATI YA HAYA MAWILI

NILIPI LA MUHIMU KWANZA KATI YA HAYA MAWILI

Ni alfajiri ya takribani saa kumi na mbili kasoro,kama ilivyo ada ninakifungulia kiredio changu ili kupata udaku unaoendelea duniani.Lakini moyoni ninahisia ya baadhi ya mambo ambayo pengine nitayasikia pindi tu nitakapo kuwa nimekifungua kiredio changu, kama matokeo ya uchaguzi wa madiwani,wabunge na raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.bila kusahau uonevu alioukili mfalme Bush dhidi ya inch ya Iraq na washukiwa wa makosa ya ugaidi.Sina wadhifa wowote katani hapa na pia si mfuasi wa chama chochote cha kisiasa ila ni mfuasi wa mgombea atakayekuwa na uchungu na inchi hii pamoja na rasilimali zilizomo na pia awe tayari kuwa kiongozi na mtumishi kwa wana inchi na asiwe mtawala.Kama ilivyo kwa wanakata wenzangu ninaamini kabisa kwamba mmoja kati ya wagombea uraisi wa chama furani lazima atashinda kiti hiki cha uraisi kwani chama chake ndicho chenye dhamana kwa sasa ya kumiliki vyombo vyote muhimu hapa inchini,kama vile jeshi,polisi na hata mahakama zote, na sababu nyingine ni mtu aliye tokea kupendwa tu jambo ambalo wengi wa wafuasi wake ukiwauliza nini alicho ifanyia Tanzania cha pekee kinacho mnusuru na dhambi walizo nazo viongozi wenzake.Lakini nimekuwa nikijiuliza bila majibu jumla ya gharama alizo zitumia bwana huyu katika kapeni yake ya uraisi ni kubwa sana ukilinganisha na ya wagombea wenzake.Najiuliza je bwana huyu akiwa raisi atakuwa na uchungu na fedha ya wanainchi?je ataweza kuwajari akina mama wajawazito na watoto dhidi ya adui mkubwa marelia?ikiwa fedha aliyo tumia kutengeneza tisheti na kofia kwa inchi nzima ingeweza kuwanunulia akinamama wajawazito vyandarua kwa inchi nzima wakiwemo watoto wa chini ya umri wa miaka mitano,hapa ninaingiwa na wasiwasi juu ya ahadi zake nyingi alizo waahidi wanainchi.Gafra ninashutka ni saa moja na kibaruani ninatakiwa kufika saa moja na nusu hivyo nina shika njia huku nikiwa ninajaribu kujihoji ni kipi cha muhimu kwanza kati uhai na kuvaa.

MIMI NAJA

Pokeeni salaam zangu mimi ni mwanablogu mpya kabisa,nimeamua kujiunga na uwanja huu ili kutoa na kuchangia machache nilio nayo.Hivyo ninapenda na kuhitaji msaada wa ushirikiano kutoka kwa wana blogu wenye mapenzi mema.